DALILI ZA KUVIMBA KWA VIFUKO VYA MAYAI YA UZAZI (OVARIAN CYST
DALILI ZA KUVIMBA KWA VIFUKO VYA MAYAI YA UZAZI (OVARIAN CYST
)
Uvimbe kwenye vifuko vya mayai ya mwanamke (ovary), hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya vifuko vya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa umri wowote ule na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito.
Sababu/ Mambo hatarishi yanayopelekea vimbe katika vifuko vya mayai: .
.
➢ Matatizo ya homoni hali hii hutokana na matumizi ya vidonge vinavyotumiwa kwa ajili ya kupevusha mayai bila ushauri wa daktari. .
.
➢ Ujauzito wakati mwingine uvimbe unaojitokeza huweza kukaa kwa kipindi cha ujauzito. .
.
➢ Endometriosis hii huwa ni hali inayosababisha seli za ukuta wa tumbo la kizazi kuota nje ya kifuko chako cha kizazi. Baadhi ya tishu zinaweza kushikamana na vifuko vyako vya mayai na kutengeneza uvimbe. .
.
➢ Kutotibu maambukizi katika mfumo wa uzazi na mkojo kama maambukizi ya bakteria kama vile UTI, fangasi, magonjwa ya zinaa kama pangusa(Chlamydia) au kisonono,
DALILI ZAKE;
. ➢ Maumivu kwenye nyonga hasa maeneo ulipo uvimbe. .
.
➢ Tumbo kujaa au kuwa zito. .
.
.➢ Tumbo kuunguruma. .
.
➢ Maumivu na kuhisi homa au kutapika. .
.
➢ Hali ya homa na uchovu kichefu chefu na kutapika .
.
.➢ Maumivu makali chini ya kitovu pembeni kushoto au kulia au pande zote. .
.
➢ Hedhi kuvurugika.
.
. ➢ Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.
Mwanamke asipotibu tatizo hili mapema anaweza kupoteza uwezo wake wa kubeba ujauzito/UGUMBA.
Wasiliana nasi kwa Ushauri na msaada Zaidi
0710 163 943 /0765 163 943

Comments
Post a Comment