DALILI ZA KUVIMBA KWA VIFUKO VYA MAYAI YA UZAZI (OVARIAN CYST
DALILI ZA KUVIMBA KWA VIFUKO VYA MAYAI YA UZAZI (OVARIAN CYST ) Uvimbe kwenye vifuko vya mayai ya mwanamke (ovary), hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya vifuko vya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa umri wowote ule na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. Sababu/ Mambo hatarishi yanayopelekea vimbe katika vifuko vya mayai: . . ➢ Matatizo ya homoni hali hii hutokana na matumizi ya vidonge vinavyotumiwa kwa ajili ya kupevusha mayai bila ushauri wa daktari. . . ➢ Ujauzito wakati mwingine uvimbe unaojitokeza huweza kukaa kwa kipindi cha ujauzito. . . ➢ Endometriosis hii huwa ni hali inayosababisha seli za ukuta wa tumbo la kizazi kuota nje ya kifuko chako cha kizazi. Baadhi ya tishu zinaweza kushikamana na vifuko vyako vya mayai na kutengeneza uvimbe. . . ➢ Kutotibu maambukizi katika mfumo wa uzazi na mkojo kama maambukizi ya bakteria kama vile UTI, fangasi, magonjwa ya zinaa kama...